Jumapili 28 Septemba 2025 - 08:03
Radi amali kali kutoka Chama cha Refah-e Melli Afghanistan dhidi ya hotuba ya Trump katika Umoja wa Mataifa

Hawza/ Chama cha Refah-e Melli Afghanistan kimekosoa vikali maneno ya hivi karibuni ya Donald Trump katika Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Mataifa kuhusu amani na kusitishwa kwa mapigano Ghaza, na kuyaita ya “uongo na kujionesha.”

Kwa mujibu wa huduma ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Chama cha Refah-e Melli Afghanistan katika tamko lake kilitoa wito kwamba; msimamo na kuingilia kati Marekani katika masuala ya nchi za Kiislamu ni “aibu kwa wananchi wa Marekani” na kikalaani vikwazo vya Magharibi dhidi ya Iran, sehemu nyingine ya tamko hilo ilielezea nia ya Marekani ya kurudisha kambi ya Bagram kama “tishio la wazi” dhidi ya muungano wa taifa la Afghanistan.

Nukuu ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:

Bismillāhi r-Rahmāni r-Rahīm

Maneno ya Trump, Rais wa Marekani, katika Mkutano Mkuu wa 80 wa Jumuiya ya Umoja wa Mataifa kuhusu amani na kusitishwa kwa mapigano Ghaza ni uongo na ya kujionesha; amani inaweza kuja duniani pale tu wahalifu kama Netanyahu na Galant, Waziri wa Ulinzi wa zamani wa Israeli, watakapoitishwa mahakamani, na pale Bwana Trump mwenyewe atakapo acha kuunga mkono na kusukuma upande wa utawala wa kigaidi wa Israel. Msimamo na kuingilia kati bila kipimo kwa Bwana Trump, Rais wa Marekani, katika mambo ya nchi za Kiislamu na mkoa, hasa Iran, ni aibu kwa watu wa Marekani.

Chama cha Refah-e Melli Afghanistan kipinga vikali vikwazo vya dhulumu vya Marekani na nchi tatu za Ulaya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kinaona kama msaada wa wazi kwa utawala wa kinyama na wa ugaidi wa Israel, nchi za Magharibi zinazofuata sera za upande mmoja za Marekani zitahisi aibu mbele ya historia na watu wao.

Chama cha Refah-e Melli Afghanistan kinapinga vikali kauli za hivi karibuni za Bwana Trump kuhusu kurudisha kambi ya anga ya Bagram na kuziona kama aina ya tishio wazi dhidi ya watu na uhuru wa nchi ya Afghanistan.

Marekani na nchi zaidi ya arobaini za Magharibi ziliishika Afghanistan kwa miaka 20 kwa kauli mbiu ya kupambana na ugaidi; walifanya uharibifu, mauaji ya watu na wizi, rasilimali na mali za watu wa Afghanistan, hakuna lililotokea linaloweza kuonekana kuwa mafanikio mengine.

Rais wa Marekani, Bwana Trump, ni mtu wa biashara na maslahi ya kifalme yanamfanya atake kuweka vituo vya kijeshi katika nchi za Kiislamu kama Afghanistan, Iraq, Umoja wa Falme wa Kiarabu, Qatar na Saudi Arabia, na lengo lake ni kuiba rasilimali na utajiri wa mataifa mengine, Marekani haiwezi kuwa mdai wa haki za binadamu; serikali ya Marekani ni miongoni mwa wakiuka haki za binadamu kwa uwazi duniani.

Katika Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1945 Marekani ndiyo iliyoangamiza miji miwili ya Japan, Nagasaki na Hiroshima, kwa shambulio la nyenzo za kwanza za nyuklia, ikaua mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia. Na pia ilikuwa Marekani mwaka 1367 (H.S) iliyopiga ndege ya abiria la Iran Air A330 na makombora mawili kutoka meli ya kivita ya Marekani (USS) juu ya anga ya Bandar Abbas na kuua abiria 290.

Na ilikuwa Marekani iliyotupia bomu la kilo tano na nusu linaloitwa “mama wa mabomu” katika mkoa wa Nangarhar Afghanistan, ambalo lilitumia tani 9 za TNT; na hii ni Marekani inayobomoa nchi za Kiislamu kama Iraq, Iran, Afghanistan, Yemen, Lebanon, Syria, Qatar, n.k. Na ni Rais wa Marekani, Bwana Trump, aliyesema: “Ikiwa tutaanza vita Afghanistan tunaweza kuimaliza ndani ya wiki moja lakini sitaki kuuawa kwa watu milioni 10.”

Kwa hivyo Marekani si wa kuaminika; kila taifa litakalomwamini Marekani litajiingiza katika udanganyifu.

Chama cha Refah-e Melli Afghanistan kinataka nchi zote za Kiarabu na Kiislamu na nchi huru za dunia zivunje kabisa uhusiano na utawala wa kinyama wa Israel.

Utawala wa kinyama wa Israel kwa mashambulizi ya mfululizo dhidi ya nchi za Kiislamu ikiwemo Iran, Qatar, Yemen, Syria, Lebanon na Ghaza umeonyesha wazi kuwa haujiamini katika kanuni, sheria na viwango vya kimataifa, na unafanya kazi kama jeshi la kikosi cha kuweka msimamo kwa ajili ya Marekani.

Was-Salāmu

Chama cha Refah-e Melli Afghanistan

Jumamosi — 5 Mizan 1404
Saturday — September 27, 2025

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha

Comments

  • Issa Hassan Ndegeya TZ 16:03 - 2025/09/29
    Trump namuona kama mtu asiyefikiri kwanza kabla ya kutenda. Ni mtuambae kusema uongo kwake siyo shida.